بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Al-Khairiya Islamic Foundation

Taasisi ya Kiislamu inayojikita katika kutoa elimu bora, kusaidia jamii, na kuendeleza maadili ya Kiislamu nchini Tanzania.

Kuhusu Sisi

Al-Khairiya Islamic Foundation imeanzishwa mnamo tarehe 28/01/2022 Tanzania ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, wilaya ya Kigamboni. Ilianza ikiwa na wanachama 16, na hadi tarehe 19/03/2023 ilifikia wanachama 31. Taasisi ilipata usajili rasmi tarehe 21/03/2025 kwa namba ya usajili S.A 23853.

Dira Yetu

Kuwa taasisi bora ya Kiislamu nchini Tanzania inayochochea maendeleo ya elimu, afya, na ustawi wa jamii kwa misingi ya Uislamu na umoja wa kijamii.

Dhima Yetu

Kutoa elimu bora ya Kiislamu, kusaidia makundi maalum kama yatima, wajane, na wazee, na kuendeleza miradi ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya jamii nzima.

Maadili Yetu
  • • Uadilifu
  • • Huruma
  • • Umoja
  • • Uwajibikaji
  • • Ubora

Uongozi Wetu

Viongozi Wakuu (2025)
  • Sheikh Ayubu Anzima Mohammed Mwenyekiti
  • Hamis Bilali Hamis Katibu Mkuu
  • Dkt Khalidi Ramadhani Faraji Makamu Mwenyekiti
  • Ustadh Abdul Mohammed Johari Naibu Katibu
  • Mohammed Ayubu Anzima Mwekahazina
  • Amina Akida Hamidu Naibu Mwekahazina
Bodi ya Wadhamini (2025)
Bodi ya Wadhamini
  • Mohammed Abdallah Sebea
  • Sheikh Ayubu Anzima Mohammed
  • Dkt Juma Nyakazilibe
  • Zakaria Mkundi
  • Bi Laila Omari Zuber
  • Bi Mariamu Khamisi Bakari

Malengo na Madhumuni

Baada ya miaka mitatu (3), tunatarajia kufikia malengo yafuatayo:

Elimu

Kujenga shule za Kiislamu kuanzia awali hadi chuo kikuu

Afya

Kuanzisha vituo vya afya na maabara

Yatima

Kuanzisha vituo vya watoto yatima

Kilimo

Miradi ya kilimo na ufugaji

Madrasa

Kujenga madrasa na misikiti

Elimu ya Dini

Kusimamia elimu ya dini na jamii

Shughuli Kuu na Mafanikio

Mashindano ya Tahfidhi Qur'an

Kusimamia mashindano ya Tahfidhi Qur'an kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa (2022-2024), na lengo la kufanya mashindano ya taifa mwaka 2025

Msaada wa Kijamii

Kutoa msaada kwa yatima, wajane, wazee, na watu wenye mahitaji maalum

Semina na Warsha

Kuandaa semina, warsha, na makongamano ya kijamii na kidini

Vyombo vya Habari

Kuanzisha na kuendeleza vyombo vya habari vya kidigitali kwa ajili ya elimu ya jamii

Mawasiliano

Tupo tayari kukusaidia. Wasiliana nasi kwa njia yoyote inayokufaa.

Tuma Ujumbe

Taarifa za Mawasiliano

Makao Makuu

Wilaya ya Kigamboni, mtaa wa Ferry
Fremu za CCM, namba 28 na 29
Dar es Salaam, Tanzania

Ona Ramani
Simu

+255 787 425 811
Mwenyekiti: Sheikh Ayubu Anzima Mohammed

Piga Simu
Masaa ya Ofisi
Jumatatu - Ijumaa: 8:00 AM - 5:00 PM
Jumamosi: 9:00 AM - 2:00 PM
Jumapili: Tumefunga

Mahali Tulipo

Bofya ramani hapo juu kupata maelekezo ya kufika ofisini mwetu